Author: super-admin

  • Watahiniwa 3,099 wakidhi vigezo vya kufanya Mtihani wa Usajili na Leseni Agosti 23, 2024

    Watahiniwa 3,099 wakidhi vigezo vya kufanya Mtihani wa Usajili na Leseni Agosti 23, 2024

    Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili TNMC Bi. Agnes Mtawa imeeleza kuwa Mtihani wa usajili na leseni unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2024. TNMC imefunga dirisha la usajili kwa watahiniwa wenye sifa za kufanya Mtihani huu, ambao hufanyika  kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya  mwaka 2010 Kifungu 6 (o) kwa lengo la kupima umahiri kabla ya kumruhusu mwanataaluma kwenda kutoa huduma kwa jamii.

    Taarifa ya msajili imeeleza kuwa Katika usajili wa watahiniwa ulioanza 01 Julai 2024 nakufungwa 14 Agosti 2024. Jumla ya watahiniwa 3,099 wamekidhi vigezo na wamesajiliwa kufanya mtihani huu. Watahiniwa hawa wanajumuisha ngazi ya Shahada 195, Stashahada 2823 na Astashahada 81.

    Bi. Mtawa katika taarifa hiyo amevitaja Vituo vya Mtihani ni kama ifuatavyo;

    1. Chuo Kikuu cha Dodoma, (College of Business – Administration And School of Law (Humanities Bondeni) Kumbi ni CAFE THEATRE 1,2,3) UDOM kilichopo Jijini Dodoma
    2. Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Mbeya iliyoko Jijini Mbeya
    3. Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT) kilichopo Malimbe Jijini Mwanza
    4. Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kilichopo Temeke jijini DSM

    Aidha katika hatua nyingine Msajili amewataka Watahiniwa wote kufika siku moja kabla ya siku ya mtihani yaani Alhamisi ya tarehe 22/08/2024 katika vituo walivyochagua kuanzia saa mbili kamili asubuhi kwaajili ya maelekezo muhimu. Siku ya ijumaa ya tarehe 23/08/2024 kila mtahiniwa anatakiwa awe amefika kwenye kituo alichochagua 07:00 asubuhi bila kukosa na ambaye hatafika atakuwa amepoteza sifa ya kufanya Mtihani. Kila Mtahiniwa anatakiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani akiwa na muonekano nadhifu na vifaa vifuatavyo:

    1. Kalamu Nyeusi (aina ya Obama) au Penseli (HB Original)
    2. Picha mbili (passport size)
    3. Kitambulisho (Indexing card,) Kwa wale wasio kuwa na Indexing kadi wanatakiwa kuja na kitambulisho cha taifa au cha mpigakura.

    Hata hiyo, Watahiniwa wanakumbushwa kuzingatia taratibu zote za mtihani na kuheshimu maelekezo ya wasimamizi uwapo chumba cha Mtihani. Pia, kujiepusha na tabia za udanganyifu kabla ya Mtihani, ukiwa katika chumba cha Mtihani na hata baada ya Mtihani, kwani ukibainika unajihusisha na udanganyifu wowote ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na kwa Mujibu wa Sheria hii adhabu yake ni kufutiwa mtihani   kwa Mujibu wa Kifungu 22 cha Kanuni.

    Mwisho; Msajili Kwa niaba ya Baraza amewatakia Safari njema watahiniwa wote kuelekea kwenye vituo vya Mtihani na amewatakia Mtihani Mwema.

  • TANZANIA TUMEJIPANGA KUUDHIBITI UGONJWA WA MPOX USIINGIE NCHINI MPOX – MHE. MHAGAMA

    TANZANIA TUMEJIPANGA KUUDHIBITI UGONJWA WA MPOX USIINGIE NCHINI MPOX – MHE. MHAGAMA

    Serikali ya Tanzania imejipanga kuudhibiti ugonjwa wa Mpox usiingie nchini kwa kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri kupitia huduma za Afya Mipakani ikiwemo bandari, nchi kavu na viwanja vya ndege, ili kubaini wasafiri wenye viashiria na dalili za ugonjwa huu na kuchukua hatua stahiki.

    Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama Jijini Dodoma akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa Ugonjwa huo ambao umetangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni tahadhari ya Afya Duniani.

    Waziri Mhagama amewatoa hofu wananchi na wataalamu wa Afya kuwa bado Tanzania iko salama juu ya ugonjwa wa Mpox hivyo kuendelea kushirikiana kuhakikisha nchi inabaki salama.

    Mhe. Mhagama ameeleza kuwa Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya nchini wamejipanga kufatilia katika jamii mtu yeyote mwenye viashiria au daliliza ugonjwa huo ili kumhudumia kwa haraka na kupunguza kusambaa kwa maambukizi endapo ugonjwa utaingia nchini.

    Mhe. Mhagama amewatoa hofu wananchi na wataalamu wa afaya kuwa bado Tanzania iko salama juu ya ugonjwa wa Mpox hivyo kuendelea kushirikiana kuhakikisha nchi inabaki salama.

    Amesema serikali imechukua hatua za kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri kupitia Huduma za Afya mipakani ikiwemo bandari,nchi kavu na viwanja vya ndege, ili kubaini wasafiri wenye viashiria na dalili za ugonjwa huo na kuchukua hatua stahiki.

    Mhe. Mhagama ameeleza kuwa Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa afya nchini wamejipanga kufatilia katika jamii mtu yeyote mwenye viashiria au daliliza ugonjwa huo ili kumhudumia kwa haraka na kupunguza kusambaa kwa maambukizi endapo ugonjwa utaingia nchini.

    Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ameeleza kuwa wataalamu wa Afya nchini wamejipanga kuweza kutoa huduma bora za matibabu kwa watu watakaobainika kuwa kuna mgonjwa wa Mpox hata hivyo wameimarisha Huduma za uchunguzi na utambuzi maeneo ya mipakani

  • Wizara ya Afya na Taasisi zake zatwaa Tuzo Maonesho ya Nanenane.

    Wizara ya Afya na Taasisi zake zatwaa Tuzo Maonesho ya Nanenane.

    Wizara ya Afya na taasisi zake imetwaa Tuzo ya Wizara Mtambuka kwa kushika nafasi ya Tatu katika Maonesho Kimataifa ya Nane Nane 2024 Jijini Dodoma.

    Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekabidhiwa siku moja kabla yakukamilika kwa Maonesho hayo yaliyohitimishwa Agosti 10, 2024.

    Wizara ya Afya pamoja na Taasisi zake imekuwa moja ya Wizara Mtambuka iliyoshika nafasi za juu kwa Ubora wa Huduma ilizo zitoa kwa takribani Siku zote za maonesho, ambapo zaidi ya wananchi wasiopungua 10,000 wametembelea Mabanda ya Wizara na kupatiwa huduma.

    Miongoni mwa huduma ambazo zimesha tolewa na zinaendelea kutolewa ni pamoja na Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi, Chanjo ya Homa ya Ini na Uviko-19, Elimu juu ya Afya ya Akili, Upimaji wa VVU/UKIMWI,Upimaji wa Kifua Kikuu ( TB ), Maleria pamoja na, Elimu kuhusu Tiba Asili na Elimu juu ya Lishe.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) limekuwa miongoni mwa taasisi za Afya zilizoshiriki maonesho hayo ya kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma likijikita katika utoaji wa elimu juu ya majukumu yanayotekelezwa na Baraza sambamba na zoezi la uhuishaji wa leseni kwa wauguzi na wakunga.

    Maadhimisho ya sherehe za Nanenane mwaka huu zibebwa na kali mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora wa Serikali ya Mtaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.

  • FAHAMU HAKI NA WAJIBU WA MGONJWA/MTEJA AKIWA KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

    FAHAMU HAKI NA WAJIBU WA MGONJWA/MTEJA AKIWA KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

    Akizungumza na vyombo vya Habari katika Maonesho ya kimataifa ya Nanenane Jijini Dodoma Afisa Uhusiano Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) Ndugu Ezekiel Nyalusi amesema jamii ni vyema ikafahamu haki na wajibu wa mteja au mgonjwa pindi anapofika kupewa huduma za Afya katika kituo cha kutolea huduma.

    Ndugu Nyalusi amzeiainisha haki hizo kuwa ni: Kupatiwa taarifa unazohitaji kuhusu ugonjwa na matibabu yako. Kupatiwa matibabu bila kukemewa, kukaripiwa au kufedheheshwa,Kupata huduma kwa wakati, kutegemea aina ya huduma, Kuwa na hiyari kupata taarifa zako za kiafya, Kupata huduma stahiki kwa makundi maalumu kama vile, Walemavu, Wazee, Wajawazito, Watoto wa chini ya miaka mitano na wenye magonjwa sugu, kutoa mrejesho wa huduma uliyopatiwa, Kufuata kanuni na taratibu za kituo husika, Kuwaheshimu watoa huduma ikiwa ni pamoja na kutumia lugha Safi, Kumueleza muhudumu wa Afya taarifa zote ambazo zitamuwezesha kutoa tiba sahihi ikiwa ni pamoja na kumpa rekodi za matibabu ya awali ulizonazo na Kutafuta matibabu kwa haraka na mapema iwezekanavyo ili wahuhudumu wa Afya waweze kukupa huduma sahihi.

    Kwa Upande wake Bi. Irene Chilewa ambaye ni Kaimu mkuu kitengo cha Udhibiti Ubora TNMC amewataka wauguzi na wakunga kufuata Kanuni za Maadili ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kuwa ni Kuheshimu Utu uhai, kupata idhini ya mteja kabla ya kutoa huduma, kutimiza wajibu wako na kuwa tayari kuwajibika kwa matendo yako, kudumisha weledi na ujiendeleze kitaaluma,kuwa mwaminifu na kutoa huduma bila upendeleo, kushirikiana na watoa huduma wengine na kufanya kazi kama timu, kutunza siri za Mteja/ Mtu unaye mhudumia.

    TNMC imeshiriki Maadhimisho ya maonesho ya kitaifa ya Nanenane kwa muda wote wa siku nane ikitoa huduma mbalimbali za Baraza kama vile Uhuishaji wa leseni, sajili na utoaji wa elimu ya sheria na maadili kwa wauguzi na wakunga na kutoa elimu ya haki ya mteja akiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya

  • Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya

    Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi kutokana na maendeleo katika Sekta hiyo.

    Rais Dkt. Samia amesema hayo Julai 31, 2024 wakati akifunga Kongamano la kumbukizi la Hayati Benjamini Mkapa kongamano ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ndani na nje ya nchi walijadili changamoto na namna ya kuzitatua katika upande wa rasilimali watu.

    “Changamoto ya upungufu wa watumishi katika Sekta ya Afya inatokana na kukua kwa idadi ya watu ambapo inapelekea kuongezeka uhitaji wa wataalamu wa afya na walimu, lakini endapo Tanzania itakua kiuchumi changamoto hiyo itaondoka.” Amesema Rais Samia

    Amesema, Suala la rasilimali watu katika Sekta ya Afya sio la Wizara ya Afya pekee bali wanaofaidika na watumishi wa Afya ni TAMISEMI na Wizara ya Afya wanasimamia Hospitali za Kanda, Mkoa pamoja na MUHIMBILI.

    Aidha, Rais Samia amesema Mafanikio katika Sekta ya Afya yanategemea na jitihada za pamoja ikiwemo Serikali, Sekta binafsi, Wadau, pamoja na Taasisi za kidini huku jukumu kubwa la Serikali ni kuweka vichocheo vya uwekezaji ili kuongeza ubora wa huduma za Afya nchini.

    Kabla ya kufunga Kongamano hilo, Rais Samia amesema Serikali ameipongeza Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kwa kujidhatiti kuboresha mifumo na nguvu kazi ya Afya kwa kuajiri watumishi wa mikataba huku baada ya mkataba kuisha wanaajiriwa na Serikali.

    Naye, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametaja maazimio ya mkutano huo kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeongeza udahili wa wanafunzi wa Taaluma za Afya ngazi ya kati, kutoka wanafunzi 20,030 mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi 25,390 ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa watumishi wa kada hiyo.

  • Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathon Dodoma.

    Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathon Dodoma.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Mapema Julai 28, 2024 ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathoni zilizoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Bank).

    Mbio hizo za Kilomita 42, 21, 10, 5 na Mbio maalum za Viongozi zimeanzia viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma na kuishi katika viwanja hivyo ilihali Shabaha yake ikiwa ni kuchangia uboreshaji wa huduma za Afya nchini, ambapo Shilingi za kitanzania Milioni 100 zitapelekwa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, Millioni 100 kutumika kusomesha wauguzi na wakunga kupitia Taasisi Benjamini Mkapa na Milioni 50 kuchangia ujenzi wa Majengo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mbali ya michango hiyo mbio hizo zinatumika kuhamasisha mazoezi ili kupambana na Magonjwa yasiyoambukiza.

    Baadhi ya Viongozi walioambatana na Waziri Mkuu ni pamoja na Naibu Waziri wa Michezo Sanaa na Utamaduni Mhe. Hamiss Mwinjuma, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt John Jingu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Mohamed Janabi, Mkurugenzi wa Huduma za kinga Ntuli Kapologwe pamoja na mamia ya wananchi kutoka ndani na nje ya nchi.

    Hata hivyo Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni miongoni mwa taasisi iliyoshiriki katika marathon kwa kuwalipia ada za ushiriki wauguzi na wakunga zaidi ya 90 kushiriki zoezi hilo.

  • ZIFAHAMU KANUNI SABA ZA MAADILI YA UUGUZI NA UKUNGA NCHINI.

    ZIFAHAMU KANUNI SABA ZA MAADILI YA UUGUZI NA UKUNGA NCHINI.

    1. Heshimu Utu uhai.
    2. Pata idhini ya mteja kabla ya kutoa huduma.
    3. Timiza wajibu wako na kuwa tayari kuwajibika kwa matendo yako.
    4. Dumisha weledi na ujiendeleze kitaaluma.
    5. Uwe mwaminifu na kutoa huduma bila upendeleo.
    6. Shirikiana na watoa huduma wengine na kufanya kazi kama timu.
    7. Tunza siri za Mteja/ Mtu unaye mhudumia.

  • MTIHANI WA USAJILI NA LESENI KUFANYIKA AUGUST 23, 2024

    MTIHANI WA USAJILI NA LESENI KUFANYIKA AUGUST 23, 2024

    Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, inawatangazia   wahitimu wote wanaotarajia kufanya mtihani wa Usajili na Leseni, kuwa mtihani unatarajiwa kutafanyika tarehe 23/08/2024.

    Kwamba, Dirisha la maombi limefunguliwa lipo wazi toka tarehe 01/07/2024 na litafungwa tarehe 14/08/2024. Maombi yote yafanyike kupitia mtandao kwa kutumia mfumo wa Baraza www.tnmcis.tnmc.go.tz

    Waombaji wote mnajulishwa kuzingatia yafuatayo;

    • Kuwa na namba ya utambulisho (Indexing Number) kwa mujibu wa kifungu cha 14 (1) cha kanuni za mafunzo.
    • Kuzingatia taratibu zote za maombi ambazo zimeambatanishwa ikiwa ni pamoja na kuweka picha sahihi (Passport Size 45X35), kujaza majina sahihi yanayoendana na vyeti vya kufunzu elimu ya Sekondari.
    • Kufanya malipo kwa wakati na kuchagua kituo sahihi cha mtihani.

    Mtihani utafanyika katika vituo vinne (4) ambavyo ni chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Jijini Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Jijini Mwanza, Taasi ya Uhasibu Mbeya, Jijinini Mbeya na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jjijini Dar es Salaam.

  • UJENZI WA OFISI ZA TNMC DODOMA WAFIKIA 59.9%

    UJENZI WA OFISI ZA TNMC DODOMA WAFIKIA 59.9%

    Menejimenti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) leo Julai 11, 2024 imefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Baraza (site visiting) kuangalia hatua za ujenzi wa Ofisi za Baraza.

    Ujenzi huo unaotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Strategic Business Solution Limited (SBS) unaendelea katika eneo la Medeli Jijini Dodoma ambapo hadi sasa umefikia asilimia 59.5%,
    ambapo mradi utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 za kitanzania.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linajenga Ofisi Kuu Jijini Dodoma hii ni baada ya maelekezo ya Serikali ya kuzitaka Taasisi zote za Umma kuhamia Makao Makuu ya nchi, awali Ofisi kuu za TNMC zilikuwa Mjini Kibaha mkoani Pwani.

  • TNMC YAHAMASISHA MAADILI, SHERIA YA UUGUZI NA UKUNGA PAMOJA HUDUMA BORA KWA WATEJA MKOANI TANGA

    TNMC YAHAMASISHA MAADILI, SHERIA YA UUGUZI NA UKUNGA PAMOJA HUDUMA BORA KWA WATEJA MKOANI TANGA

    Kikosi cha Maafisa kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) kipo mkoani Tanga kwaajili ya kuhamasisha Maadili, Sheria ya Uuguzi na Ukunga na huduma bora kwa wateja.

    Pamoja na shughuli hizo watatembelea vyuo vya Uuguzi na Ukunga ili kujionea hali halisi ya utoaji wa Mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kusisitiza uzingatiaji wa miongozo.