Author: super-admin

  • TNMC NA UKUSANYAJI WA MAONI YA SHERIA YA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA.

    TNMC NA UKUSANYAJI WA MAONI YA SHERIA YA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA.

    Baraza la uuguzi na ukunga Tanzania TNMC, limeendelea kukusanya maoni kwa wauguzi na wakunga wa Halmashauri za Wilaya za Wanging”ombe na Makete mkoani Jombe, zoezi hili linalengo la kuihuisha ili kuiboresha Sheria ya uuguzi na ukunga ya Mwaka 2010.

    Wakizungumza katika vikao maalumu vya kukusanya maoni hayo, wanataaluma hao wametoa maoni ya kuboresha Sheria hiyo katika vipengele mbalimbali ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa vituo binafsi vya kutolea huduma za uuguzi na ukunga, makosa ya kitaaluma na athabu zake pamoja na Suala la leseni kwa wanataaluma wa kada hiyo.

    Sheria inayosimamia taaluma na wanataaluma wa kada za uuguzi na ukunga ilitungwa kwa mara ya kwanza mwaka 1952 kabla ya kuhuishwa mwaka 1997 na kisha kutungwa mpya mwaka 2010 ambapo maoni yanayotolewa yanalengo la kuihuisha ili iendane na wakati uliopo.

  • TNMC YAWATUNUKU VYETI NA LESENI WAUGUZI NA WAKUNGA WAPYA 415.

    TNMC YAWATUNUKU VYETI NA LESENI WAUGUZI NA WAKUNGA WAPYA 415.

    • Mwenyekiti wa baraza alitaka baraza kuendelea kusimamia viwango vya taaluma
    • Muuguzi Mkuu wa Serikali awakaribisha Wauguzi na Wakunga wapya katika kada ya Afya.

    Wauguzi na wakunga wapya 415 wametunukiwa vyeti na usajili na leseni katika Mahafali ya 11 ya kitaaluma  jijini Dodoma.

    Akifungua Mahafali hayo Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Prof. Lilian Msele ameipongeza Menejimenti ya Baraza kwa maandalizi ya mahafali hayo huku akiwataka wauguzi na wakunga wapya kwenda kuitumikia jamii kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu.

    Katika hatua nyingine Prof. Msele amewataka wauguzi viongozi kusimamia vyema huduma za Uuguzi na Ukunga hapa nchini

    ”Hivi siku za karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya wateja juu ya huduma za Uuguzi na Ukunga, Nitumie fulsa hii kuwataka wauguzi viongozi kusimamia vyema maadili kwa wauguzi na wakunga hapa nchini ili kuweza kupunguza malalamiko mengi ya wateja katika jamii” alisema Prof Mselle.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga Tanzania na Muuguzi Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amewapongeza wauguzi na wakunga wapya kwa kuhitimu masomo na amekaribisha katika kada ya Afya huku akiwataka kuendelea kuzingatia maadili ya taaluma.

    “Nipenda kauli mbiu inayosema Wauguzi na wakunga ni watu maalumu kwa kazi maalum, hivyo tujivunie taaluma yetu, sasa mmemaliza kupewa leseni na baraza mimi nawapokea katika kada ya Afya ila mkifanya makosa ya kitaaluma mimi nitawarudisha kwenye baraza” alisema Bi. Lilian

    Naye Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadli Bi. Jane Mazigo amebainisha idadi ya wauguzi na wakunga waliosajiliwa na kupewa leseni ni wamefikia 52,188 hapa nchini huku baraza liliendelea kusimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini ili jamii iweze kupata huduma iliyobora salama.

    Hata hivyo, Baadhi ya wauguzi na wakunga wameahidi kwenda hudumia jamii kwa kufuata sheria taratibu na miongozo yote ya Afya hapa nchini.

  • WAUGUZI, WAKUNGA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI KUEPUKA MAAMBUKIZI.

    WAUGUZI, WAKUNGA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI KUEPUKA MAAMBUKIZI.

    Bi.Salome Kassanga Mkufunzi wa Mafunzo ya chumba cha Upasuaji na Afisa Mwandamizi kutoka TNMC ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Pwani, wakishirikiana na wadau wa Shirika la Korea Foundation for International Health Care (KOFIH) wakiwa na lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na watoto wachanga.

    “Ni muhimu kufuta taratibu za chumba cha Upasuaji kuepuka maambukizi kutokana mpangilio mzuri wa chumba cha upasuaji, Mazingira Rafiki hasa vifaa viwe safi muda wote” alisema Bi Kassanga.

    Kwaupande wake muwezeshaji Dokta Alfonce Moyo Kutoka hospitali ya Tumbi amebainisha umuhimu wa kushirikiana kama timu wakati wautoaji huduma katika chumba cha upasuaji na kusema ushirikiano huo unaleta tija na ufanisi wa utendaji kazi hasa kwenye chumba cha upasuaji.

    “Mara nyingi watu hawafahamu suala la utoaji huduma katika chumba cha upasuaji wanadhani anahusika Daktari pekee, kumbe asilimia kubwa Muunguzi ndiye wa kwanza kuandaa mazingira yote ya huduma hii lakini mimi niseme kitu hapa ni muhimu umma ukafahamu kuwa sisi tunafanya kazi kama timu, mteja yule ni wetu sote hivyo kila mmoja wetu anajukumu la kumuhudumia ipasavyo hivyo mafunzo haya yataleta sura mpya ya kushirikiana kikamilifu katika utoaji huduma hii” alisema Dkt. Moyo

    Naye, Dkt. Tanya Mahalo, Mtaalamu wa dawa ya Usingizi na ganzi kutoka hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, amesema ni vyema kuanza kumuandaa mgonjwa nje ya chumba cha upasuaji kwa kumpa taarifa sahihi ya huduma ipi anayoenda kuipokea, na baada ya kupata huduma lazima awe chini ya uangalizi maalumu mpaka atakapo pata nafuu, ameongeza kuwa ni vizuri tukamuhudumia mteja kwa upendo hasa awapo katika kituo cha kupokea huduma.

    Mafunzo yameanza tarehe 08 Aprili 2024 na yanatarajiwa kutamatija tarehe 04 Mei 2024 katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha DC, Kibaha TC, Kisarawe, Kibiti na Rufiji.

  • MSAJILI TNMC AMEWAPONGEZA WAUGUZI VIONGOZI KWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO

    MSAJILI TNMC AMEWAPONGEZA WAUGUZI VIONGOZI KWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO

    Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi viongozi kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika utendaji wa majukumu ya Baraza katika maeneo yao ya kazi.

    “Nitumie fulsa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya huko kwenye maeneo yenu ninyi ni wasaidizi wangu, fanyeni kazi kupunguza malalamiko ya wateja pia simamieni vyema wauguzi watarajali na wale wanao wabeza waleteni huku Barazani tutawashughulikia kwa mujibu wa Sheria”-

    Bi.Mtawa ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

    Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinajali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

    Mkutano huu unafanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024 Umebebwa na Kauli mbiu “Huduma sitaha na mawasiliano Madhubuti ni wajibu wa kila mtoa huduma za Afya”

  • TUTATUE MIGOGORO MIDOGOMIDOGO KAZINI KWETU

    TUTATUE MIGOGORO MIDOGOMIDOGO KAZINI KWETU

    Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania(TANNA) Bwana Alexanda Balulya, amesema kuna umuhimu wa kushirikiana katika utendaji kazi wawapo vituo vya kazi na kuiheshimu tasnia ya Uuguzi na Ukunga nchini. “Ubaguzi wakitaaluma hautakiwi katika utendaji kazi, tutunziane heshima na mapungufu ya kitaaluma huku tukiitatua migogoro midogo midogo katika tasnia yetu tusikimbilie kwenye vyombo vya habari” amesema Bwana Balulya.

    Ameyasema hayo Rais wa TANNA akichangia hoja wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

    Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya.

    Mkutano huu unafanyika Jijini Dodoma katika kuanzia tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024 Umebebwa na Kauli mbiu “Huduma Sitaha na Mawasiliano Madhubuti ni wajibu wa kila mtoa huduma za Afya”

  • NI LAZIMA TUZALISHE WAUGUZI NA WAKUNGA WENYE WELEDI

    NI LAZIMA TUZALISHE WAUGUZI NA WAKUNGA WENYE WELEDI

    “Ilituweze kuboresha huduma ya jamii inatakiwa kuwa na wauguzi wenye sifa ya kuhudumia jamii, “ni kweli tukubali kuwa tupo na shida ya walimu wasio na sifa ya kufundisha wanafunzi haiwezekani mwalimu umetoka chuo ukaenda kufundisha wanafunzi wakati hujawahi kufanya kazi kwa vitendo” Bi. Ziada.

    Bi.ziada ameongeza kuwa kuna umuhim mkubwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kukaa pamoja na NaCTE na wadau wengine wa elimu ya kuona namna bora ya kuweka utaratibu mzuri wa utoaji mafunzo ya kada ya Uuguzi na Ukunga Tanzania.

    Muuguzi mkuu wa serikali Bi.Ziada Sellah ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

    Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

    Mkutano huu unafanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024 Umebebwa na Kauli mbiu “Huduma sitaha na mawasiliano Madhubuti ni wajibu wa kila mtoa huduma za Afya”

  • TNMC: WAUGUZI VIONGOZI SIMAMIENI VYEMA MAADILI KATIKA VITUO VYENU.

    TNMC: WAUGUZI VIONGOZI SIMAMIENI VYEMA MAADILI KATIKA VITUO VYENU.

    Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadili kutoka TNMC Bi. Jane Mazigo amewataka Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini kusimamia vyema huduma za Afya nchini sambamba na kuhakikisha huduma ya Uuguzi na Ukunga zinafuata Maadili, taratibu na miongozo ya huduma ya Afya.

    Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

    Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

    Mkutano huu unafanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa PSSSF tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024

  • TNMC:WAUGUZI, WAKUNGA WALIOSAJILIWA WAFIKIA 52,000.

    TNMC:WAUGUZI, WAKUNGA WALIOSAJILIWA WAFIKIA 52,000.

    Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Bi. Agnesi Mtawa, leo amefanya mahojiano na shirika la Utangazaji Tanzania TBC Kupitia kipindi cha Asubuhi kinachofamika kwa jina la Jambo Tanzania.

    Akizungumza katika mahojiano hayo maalum yenye lengo la kuangazia mafanikio ya Baraza kuelekea maadhimisho ya miaka 71 tangu kuanzishwa mwaka 1953, Msajili ametaja baadhi ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa ikiwa ni pamoja na; Kukua kwa Baraza na kufikia hadhi ya Taasisi ya Serikali nyenye Muundo wake wa kiutumishi ukiainisha kurugenzi, Sehemu na Vitengo vya Taasisi.

    Kuongezeka kwa idadi ya wanataaluma wa kada ya Uuguzi na Ukunga kutoka watumishi wachache mwaka 1953 mpaka watumishi 52,000 mwaka 2024, ambao wamegawanyika katika ngazi za Elimu kuanzia Astashahada mpaka Shahada ya uzamivu (Phd) na kundi kubwa ni ngazi ya Stashahada ambao ni 26, 450.

    Kuanzishwa kwa mfumo wa kielekitronoki wa kutunza orodha na taarifa za wauguzi na wakunga kote nchini, ambapo hapo awali orodha ilikuwa inatunzwa kwenye daftari la nakala ngumu ambalo lilifahamika kama Kalamazoo.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga linatarajia kutimiza miaka 71 ifikapo Jummanne ya tarehe 19/03/2024

  • Wauguzi, wakunga 2099 watunukiwa vyeti, leseni za kitaaluma.

    Wauguzi, wakunga 2099 watunukiwa vyeti, leseni za kitaaluma.

    Wauguzi na wakunga wapya wapatao 2099 wamekula kiapo cha kuitumikia taaluma hiyo kwa kuzingatia maadili, miiko, sheria na kanuni za uuguzi na ukunga.

    Wamefikia hatua hiyo baada ya kufaulu mtihani wa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) uliofanyika Desemba 29, 2023 na hivyo kupata sifa za kuorodheshwa, kusajiliwa na kupewa leseni za kutambuliwa rasmi kama wataalamu wa kada ya uuguzi na ukunga nchini.

    Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Tumaini Nagu ameshuhudia leo jijini Dodoma wauguzi hao na wakunga wakiapishwa katika mahafali ya 10 ya Kitaaluma yanayoratibiwa na TNMC.

    Kati yao, 346 ni wa shahada ya kwanza, 1737 ni ngazi ya stashahada huku 16 wakiwa ni ngazi ya astashahada.

  • Katibu Mkuu Jingu; Wasajili Simamieni Maadili Katika Kada ya Afya

    Katibu Mkuu Jingu; Wasajili Simamieni Maadili Katika Kada ya Afya

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jonh Jingu, amewaagiza Wasajili wa Mabaraza na Bodi za kitaaluma zilizochini ya Wizara ya Afya, kuimarisha na kusimamia mifumo ya Maadili ya kitaaluma na ya kazi kwa watumishi wa kada ya Afya, kwa kufika katika maeneo yao ya kazi badala ya kusubiri waletewe kesi mezani.

    Katibu Mkuu, ametoa rai hiyo Februari 02.2024 alipofanya kikao kazi na Wasajili wa Mabaraza 12 na Bodi mbili zinazosimamia Taaluma na wanataaluma wa kada mbalimbali za Afya ikiwa ni pamoja na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania(TNMC).

    “Nendeni field, tuwe na mikakati ya kuwafikia watu wetu, fuatilieni namna ambavyo wanafanya kazi, kunabaadhi ya wataalamu wetu ni watukutu, hawazingatii Maadili kama vile kutibu kinyume na tiba inayotakiwa, kutoa siri za wagonjwa, lakini pia tuimarishe mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma kwa wataalamu wetu wakiwa kazini (CPD), tusisubiri matatizo yatokee, tuwe (proactive)” alisistiza Katibu Mkuu.

    Akizungumzia suala la ugatuaji wa madaraka, Katibu Mkuu Dkt. Jingu, amewataka Wasajili hao kugatua Madaraka kwa wasimamizi wa ngazi za mikoa RNO na RMO ili kupata usimamizi wa karibu katika kusimamia Taaluma na wanataaluma, lakini pia kuwajengea uwezo ili wawe na weledi na maarifa sahihi ya kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufasaha.

    “Lakini pia, tujitangaze ili tufahamike, tuhakikishe kuwa mabaraza yetu yanajulikana kwa umma, tujitangaze kwa kufafanua majukumu yetu ili wananchi watufahamu na wanapokuwa na jambo wajue wapi pakwenda” alitanabaisha.

    Akihitimisha hotuba yake, amesema, pamoja na kwamba Mabaraza haya ni Mamlaka za kisheria, hazitakiwi kuwa kero kwa wawekezaji waliowekeza au wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Afya kwani Serikali imekuwa ikihamasisha uwekezaji katika Sekta hiyo, hivyo utekelezaji wa majukumu yao usiwe kero ya kuwakatisha tamaa.