Author: super-admin
-

NAMBA ZA MTIHANI WA USAJILI NA LESENI DISEMBA 2024.
A: BACHELOR
BACHELOR OF SCIENCE IN MIDWIFERY (KITUO CHA:KAMPALA,RUCU,IAA,UDOM,TANDABUI)
BACHELOR OF SCIENCE IN NURSING (KITUO CHA: KAMPLA,IAA,RUCU,UDOM,TPC,TANDABUI)
BACHELOR OF SCIENCE IN NURSE ANAESTHESIA (KITUO CHA: KAMPALA)B:DIPLOMA
INSTITUTE OF ACCOUNTACY ARUSHA: MAIN HALL 2
KAMPALA UNIVERSITY: LECTURE HALL 8
RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY -IRINGA: MAIN HALL 1
ST. JOHN’S UNIVERSITY OF TANZANIA: MAIN HALL (BASH)
TABORA POLYTECHNIC COLLEGE : DIAMOND HALL
THE UNIVERSITY OF DODOMA- AUDITORIUM COLLEGE OF INFORMATICS
C: CERTIFICATE
-

WAUGUZI NA WAKUNGA ZAIDI YA 1200 WATUNUKIWA VYETI NA LESENI ZA KITAALUMA.
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewatunuku wauguzi na wakunga 1222 Leseni na vyeti vya kitaaluma hii leo 13.12.2024 katika Mahafali ya 12 ya kitaaluma yaliyofanyika katika ukumbi wa st.peter’s swaswa uliopo Jijini Dodoma.
Akihutubia katika hafla ya kitaaluma Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na ukunga nchini na Muuguzi Mkuu wa Serikali Bi.Ziada sellah amewataka wauguzi na wakunga hao kuzingatia maadili ya Uuguzi na Ukunga hapa nchini kwa kufuata miongozo ya kitaaluma.
“sasa leo mmeshatunukiwa vyeti na leseni hatutegemei muuguzi na mkunga kufanya mambo kinyume na miongozo ya kitaaluma mkaihudumie jamii kwa kutoa huduma zenye utu na staha” alisema Bi. Ziada
Katika hatua nyingine Muuguzi Mkuu wa serikali amesisitiza umuhimu wa wataaluma hao kujiendeleza kitaaluma kwani taaluma ya Uuguzi na Ukunga inakuwa kila uchwao.
Naye Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Bi. Agnes Mtawa amesisitiza kwa wauguzi na wakunga kufanya kazi kwa kuzingatia mawanda yao ya kazi, huku akisisitiza kuwa na lugha nzuri wakati wa utoaji huduma za Uuguzi na Ukunga.

“sasa isiwe unafika kwa mgonjwa amelala wewe unamchoma sindano akishituka unamwambia tulia… ulikuwa hujui ni mud awa sindano? Mimi nasema ni vizuri kuwa na lugha nzuri na wateja wetu wakati wa utoaji huduma.” Alisema Bi.Mtawa
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa usajili,leseni na Maadili Bi.Jane Mazigo Pamoja na kusisitiza misingi ya maadili kwa wataaluma amewataka wauguzi na wakunga kutumia muda wao mwingi kujifunza ili kuwa wabobezi katika taaluma ya Uuguzi na Ukunga.

-

ORODHA YA WATAHINIWA NA VITUO KWA MTIHANI WA VITENDO WATAALAMU WA DAWA YA USINGIZI NA GANZI (NURSE ANAESTHETIST)
GUSA LINK HAPA CHINI KWA KITUO CHA MLOGANZILA
Orodha ya watahiniwa watakaofanya mtihani kituo cha MLOGANZILA
GUSA LINK HAPA CHINI KWA KITUO CHA UPANGA
-

WATOA HUDUMA CHUMBA CHA UPASUAJI MTWARA-SZRH WANUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA TNMC.
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limetoa mafunzo elekezi kwa Madaktari, wauguzi,wakunga na wauguzi wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi wanaofanya kazi katika vyumba vya upasuaji pamoja na baadhi ya watumishi kutoka vitengo mbalimbali vya kutolea huduma wapatao 45 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, juu ya namna bora ya kutoa huduma katika chumba cha Upasuaji “Theatre Management” kwa lengo la kumlinda mgonjwa kuwa salama baada ya upasuaji.

Mafunzo yanayodumu kwa muda wa siku 14 yanaongozwa na Afisa Muuguzi Mbobezi kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Salome Kassanga akisaidiana na Muuguzi mbobezi katika chumba cha upasuaji Bi Happiness Liya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Ligula.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga amesema kuwa, lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madaktari, Wauguzi, Wakunga na Wataalamu wengine katika chumba cha Upasuaji ili kuboresha huduma kwenye chumba cha Upasuaji na kukidhi viwango vya Kimataifa. “Tunatoa mafunzo haya ili kuhakikisha kuwa vyumba vya upasuaji kunakuwa na misingi bora ya usimamiaji na uendeshaji, misingi ya kudhibiti maambukizi kwa wagonjwa (IPC), uzingatiaji wa Maadili, Sheria, kanuni na miongozo katika chumba cha upasuaji, uvaaji wa sare maalumu za chumba cha upasuaji kulingana na miongozo husika, uzingatiaji wa kuweka taarifa za wagonjwa wanaopatiwa huduma za upasuaji (Documentation), pamoja na kulinda usalama wa mgonjwa na watoa huduma” alisema Bi. Kassanga.

Hata hivyo, Bi. Kassanga ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha watumishi juu ya utoaji wa huduma kwa kuzingatia Maadili, Miiko, Uadilifu, ikiwa ni Pamoja na uvaaji wa Sare maalumu za chumba cha upasuaji kulingana na miongozo husika, uzingatiaji wa kuweka taarifa sahihi za wateja wanaopatiwa huduma (Documentation), pamoja na kulinda usalama wa mgonjwa na watoa huduma” alisema Bi. Kassanga.
















