THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

WAZIRI MCHENGERWA: WAGONJWA WANAHITAJI FARAJA KUTOKA KWA WAUGUZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wauguzi kula kiapo cha utoaji wa huduma bora ikiwa ni pamoja na kuwapa wagonjwa faraja na msaada wa saikolojia.”Msiondoke hapa mpaka mle kiapo cha kutoa huduma bora kwa niaba ya wauguzi wengine wote walioko kwenye vituo vya kutolea huduma […]

MAJALIWA: WAKUNGA ZINGATIENI WELEDI KWENYE UTOAJI WA HUDUMA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakunga na wataalamu wengine wa afya nchini kufanya kazi kwa weledi na kuongeza bidii katika kutoa huduma kwa wananchi wanaowahudumia. Amesema kuwa kada zote za afya zinasimamiwa na miiko na maadili ya taaluma na miongozo iliyowekwa. “Hivyo basi kila mmoja ahakikishe anazingatia maelekezo mahsusi ya utendaji wa kazi.” […]

Heri ya siku ya wafanyakazi Duniani / Mei Mosi 2024

Wafanyakazi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) wameshiriki Katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na kinga […]

TNMC NA UKUSANYAJI WA MAONI YA SHERIA YA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA.

Baraza la uuguzi na ukunga Tanzania TNMC, limeendelea kukusanya maoni kwa wauguzi na wakunga wa Halmashauri za Wilaya za Wanging”ombe na Makete mkoani Jombe, zoezi hili linalengo la kuihuisha ili kuiboresha Sheria ya uuguzi na ukunga ya Mwaka 2010. Wakizungumza katika vikao maalumu vya kukusanya maoni hayo, wanataaluma hao wametoa maoni ya kuboresha Sheria hiyo […]

TNMC YAWATUNUKU VYETI NA LESENI WAUGUZI NA WAKUNGA WAPYA 415.

Wauguzi na wakunga wapya 415 wametunukiwa vyeti na usajili na leseni katika Mahafali ya 11 ya kitaaluma  jijini Dodoma. Akifungua Mahafali hayo Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Prof. Lilian Msele ameipongeza Menejimenti ya Baraza kwa maandalizi ya mahafali hayo huku akiwataka wauguzi na wakunga wapya kwenda kuitumikia […]

WAUGUZI, WAKUNGA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI KUEPUKA MAAMBUKIZI.

Bi.Salome Kassanga Mkufunzi wa Mafunzo ya chumba cha Upasuaji na Afisa Mwandamizi kutoka TNMC ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Pwani, wakishirikiana na wadau wa Shirika la Korea Foundation for International Health Care (KOFIH) wakiwa na lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na watoto wachanga. “Ni muhimu kufuta taratibu […]

MSAJILI TNMC AMEWAPONGEZA WAUGUZI VIONGOZI KWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi viongozi kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika utendaji wa majukumu ya Baraza katika maeneo yao ya kazi. “Nitumie fulsa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya huko kwenye maeneo yenu ninyi ni wasaidizi wangu, fanyeni kazi kupunguza malalamiko ya wateja pia simamieni vyema wauguzi […]

TUTATUE MIGOGORO MIDOGOMIDOGO KAZINI KWETU

Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania(TANNA) Bwana Alexanda Balulya, amesema kuna umuhimu wa kushirikiana katika utendaji kazi wawapo vituo vya kazi na kuiheshimu tasnia ya Uuguzi na Ukunga nchini. “Ubaguzi wakitaaluma hautakiwi katika utendaji kazi, tutunziane heshima na mapungufu ya kitaaluma huku tukiitatua migogoro midogo midogo katika tasnia yetu tusikimbilie kwenye vyombo vya habari” amesema […]

NI LAZIMA TUZALISHE WAUGUZI NA WAKUNGA WENYE WELEDI

“Ilituweze kuboresha huduma ya jamii inatakiwa kuwa na wauguzi wenye sifa ya kuhudumia jamii, “ni kweli tukubali kuwa tupo na shida ya walimu wasio na sifa ya kufundisha wanafunzi haiwezekani mwalimu umetoka chuo ukaenda kufundisha wanafunzi wakati hujawahi kufanya kazi kwa vitendo” Bi. Ziada. Bi.ziada ameongeza kuwa kuna umuhim mkubwa Baraza la Uuguzi na Ukunga […]

TNMC: WAUGUZI VIONGOZI SIMAMIENI VYEMA MAADILI KATIKA VITUO VYENU.

Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadili kutoka TNMC Bi. Jane Mazigo amewataka Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini kusimamia vyema huduma za Afya nchini sambamba na kuhakikisha huduma ya Uuguzi na Ukunga zinafuata Maadili, taratibu na miongozo ya huduma ya Afya. Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi […]