Author: super-admin

  • DKT. NTULI AIBUKA MSHINDI UKURUGENZI MKUU ECSA-HC

    DKT. NTULI AIBUKA MSHINDI UKURUGENZI MKUU ECSA-HC

    Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dkt. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

    Dkt. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.

    Dkt. Ntuli Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo, ataongoza kwa muda wa miaka mitano.

    Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uchaguzi Februari 12, 2025, Waziri wa Afya nchini Tanzania Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa nafasi hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba (7) walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.

    Waziri Mhagama amesema mara baada ya usaili uliofanywa na Kamati ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa nchi wanachama, Dkt. Kapologwe alipata alama za juu zaidi na kuingia katika hatua ya mwisho pamoja na wagombea wengine wawili kutoka Kenya na Malawi.

    Ameeleza kuwa majina ya wagombea hao watatu yaliwasilishwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC), ambapo Dkt. Kapologwe ameibuka mshindi.

    Kwa ushindi huu ni dhahiri ya kwamba Tanzania inaendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa ina Watalaam wenye sifa stahiki za kushika hatamu za Uongozi kwenye Jumuiya au Mashirika ya Kimataifa na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya wengi katika uboreshaji wa huduma za Afya.

    “Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushika nafasi hii katika kipindi cha miaka 51 cha Jumuiya hiyo, kwani kwa mara ya kwanza, Mtanzania Dkt. Winny Mpanju alihudumu kama Mkurugenzi Mkuu kati ya mwaka 1983 na 2000. Ni mafanikio makubwa kuona Tanzania inapata nafasi hii tena baada ya miaka 27,” amesema Waziri Mhagama.

    Jumuiya ya ECSA-HC ilianzishwa mwaka 1974 na inajumuisha nchi tisa (9) ambazo ni Tanzania, Malawi, Kenya, Lesotho, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Uganda pamoja na Eswatini na inashirikiana na nchi 13 zisizo wanachama ambazo ni Botswana, Burundi, Cameroon, Eritrea, Gabon, Liberia, Msumbiji

  • Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) wametembelea Ofisi ya Msajili -TNMC

    Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) wametembelea Ofisi ya Msajili -TNMC

    Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) wametembelea ofisi ya msajili kufahamu utendaji kazi wake hususaji kuhusu sajili za wauguzi na wakunga hapa nchini wakiwa kama wadau katika utoaji wa huduma za kiafya hapa nchini.

    Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) ni akika nani?

    Hili ni Shirika lisilo la kiserikali na la kimataifa linaoundwa na Madaktari na wafanyakazi wa sekta ya Afya.

    Pia linapokea wafanyakazi kutoka kwenye taaluma zingine ikiwemo wauguzi na wakunga ambao wanaweza kusaidia kutimiza malengo ya shirika. Wafanyakazi wake wote wanakubali kuheshimu sheria na kanuni:

    MSF inatoa msaada kwa watu walio kwenye shida, walioathirika na majanga ya asili au ya kibinadamu na waathirika wa vita. Na wanafanya hivyo bila ya ubaguzi wa rangi,dini au misimamo ya kisiasa MSF inafanya kazi bila kuegemea upande wowote kwa mujibu wa maadili ya kitabibu na haki ya msaada wa kibinadamu, shirika hili lina uhuru wa kutosha katika kufanya kazi zake.

    Hata hivyo, Wafanyakazi wa MSF wanatakiwa kuheshimu maadili ya kitaaluma na kulinda uhuru wake dhidi ya ushawishi wa kisiasa, kidini na kiuchumi. Wafanyakazi wanazoweza kukabiliana nazo wawapo kwenye kazi zao na hawapaswi kuomba malipo yoyote ya fidia zaidi ya yale ambayo MSF inaweza kuwalipa.

  • MSAJILI TNMC: INDEXING NI SUALA LA KISHERIA SI MATAKWA YA MTU BINAFSI

    MSAJILI TNMC: INDEXING NI SUALA LA KISHERIA SI MATAKWA YA MTU BINAFSI

    Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Agness Mtawa amewataka wanafunzi wote wa kada ya Uuguzi na Ukunga nchini kuhakikisha wanakamilisha   usajili wa awali (Student Indexing) ili kuweza kutambulika na mfumo wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.

    Hayo ameyasema leo wakati wa kikao kifupi walichokiomba wanafunzi wa  kada ya uuguzi na Ukunga wa chuo St. John na Ofisi ya Msajili kikao ambacho kimefanyika chuoni hapo jijini Dodoma.

    Akitaja umuhimu wa usajili wa awali Msajili amesema ni Kurahisisha ufuatiliaji wa wanafunzi waliodahiliwa na wanaoendelea na mafunzo katika vyuo, Kurahisisha mchakato wa  usajili baada ya kuhitimu mafunzo, Hurahisisha  ufuatilia wa maendeleo ya mafunzo vyuoni na kutoa takwimu ya wanafunzi wanaostahili kufanya mtihani wa leseni na usajili na kujua hali ya udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Uuguzi na Ukunga

    Aidha,  Msajili amesisitiza kuwa, Usajili wa awali (student indexing) si kwa ajili ya kupata kibali cha kufanya mtihani wa Usajili na Leseni tu bali ni zoezi muhimu linalomwezesha mwanafunzi kufanyiwa uhakiki wa sifa za kujiunga na masomo ya Uuguzi na Ukunga kisha  kupata/kutopata kibali cha kuendelea na masomo yake.

    Hata hivyo, Wadahiliwa ambao orodha/taarifa zao hazijawasilishwa Baraza hawataweza kufanya usajili huu, Sambamba na hilo, mwanafunzi atapata kadi ya usajili wa awali (indexing card) itakayotumika kwa kipindi chote cha uanafunzi na wakati wa mtihani wa Usajili na leseni.

    Ikumbukwe kuwa,  utaratibu wa kujisajili ni kuingia kwenye tovuti ya Baraza kwa kuandika neno TNMCIS au www.tnmc.go.tz Baada ya kuingia kwenye ukurasa huu wa Baraza bofya TNMCIS login utaona ukurasa huu na Bofya “click here to register” kwa waombaji wapya ambao hawana akaunti Baraza Kwa sasa maombi mengi kupitia Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania yanafanyika kwa njia njia mtandao. Hivyo mwombaji anawajibika kuchagua ombi sahihi kwa wakati huo kama ambavyo ukurasa hapo juu unavyoonyesha.

    Kumbuka: kwa wanafunzi wenye akaunti tayari kwenye mfumo wa Baraza hawatakiwi kujisajili tena bali wanatakiwa kuingia moja kwa moja kwenye mfumo (login) kwa kuweka barua pepe na nywila tu kisha kuendelea na kukamilisha maombi.

  • CHAMA CHA WAKUNGA TANZANIA (TAMA) CHAPATA ITHIBATI UTOAJI WA MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA (CPD)

    CHAMA CHA WAKUNGA TANZANIA (TAMA) CHAPATA ITHIBATI UTOAJI WA MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA (CPD)


    Kwa niaba ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Mkunga Mbobezi na Mratibu wa Mafunzo ya Kujiendeleza Kitaaluma Bi. Mwajuma Mutabazi amekabidhi Cheti cha ithibati ya Moduli sita za mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma (CPD) eneo la huduma za dharula kwa wajawazito (Midwifery Emergency Skills Training) kwa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambapo amekitaka chama hicho kusimamia misingi ya kitaaluma huku akiahidi kuwa, Ofisi ya msajili ipo wazi muda wote kutoa ushirikiano.

    Akipokea cheti hicho rais wa TAMA katika ofisi za chama hicho jijini Dar es salaam, Dkt. Beatrice Mwilike amemshukuru Msajili kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuhakikisha Moduli za mafunzo zinazowasilishwa katika Ofisi yake zinafanyiwa kazi kwa wakati hivyo kurahisisha utekelezwaji wa mafunzo yenye lengo la kuwawezesha wataaluma wa kada ya Ukunga kupata maarifa mapya yatakayowawezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii hususani katika eneo la Mama na mtoto.

    Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TAMA Bwana Nicodem Komba ameshukuru ushirikiano ulipo baina ya chama hicho cha kitaaluma na mamlaka ya usimamizi ambayo ni Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.

    Naye mshauri wa huduma za Ukunga kutoka TAMA Bi. Martha Rimoy pamoja na Katibu Mwenezi wa chama hicho Bi. Agness Nduguru kwa pamoja wameshukuru kupata cheti hicho huku wakiahidi kutoa mafunzo bora ambayo yamethibitishwa na Baraza kwa wakunga wote nchini ambayo licha ya kutoa huduma zenye viwango pia yatawaongezea alama wakati wa uhuishaji wa leseni zao.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania chini ya Sheria na. 1 ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) na Kanuni zak ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.

  • BARAZA LATANGAZA MATOKEO YA  MTIHANI WA  WA USAJILI NA LESENI, UFAULU NI  64%

    BARAZA LATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA WA USAJILI NA LESENI, UFAULU NI 64%

    Akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani huu, tarehe 23 Januari, 2025, Jijini Dodoma, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Agnes Mtawa, amebainisha kuwa, jumla ya watahiniwa 5125 walifanya mtihani huu, ambapo watahiniwa 3281 (64%) wamefaulu mtihani na watahiniwa 1844 (36%) hawakuweza kufikia kiwango cha ufaulu kinachokubalika.

    Aidha, Matokeo hayo yanapatikana kwenye akaunti ya kila mtahiniwa iliyopo kwenye mfumo wa kumbukumbu wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMCIS), Hivyo, kila mtahiniwa anatakiwa kuingia katika mfumo wa Baraza https://tnmcis.tnmc.go.tz. na kuweza kuona matokeo yake.

    Mtihani wa usajili na leseni ni kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya Uuguzi na Ukunga “The Nursing and Midwifery Act, 2010” Kifungu cha (6) (a) na (o) iliyounda Baraza la Uuguzi na ukunga nchini
    Baraza linawapongeza wale wote waliofaulu na kupata sifa za usajili na leseni na kwa wale walioshindwa kufikia viwango vya ufaulu vinavyokubalika, watajulishwa muda wa kurudia mtihani huu.

    Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TMNC ni mamlaka ya kisheria inayosimamia wanataaluma na taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na kanuni zake ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini zina kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.

  • WAUGUZI, WAKUNGA WAKUMBUSHWA JUU MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA.

    WAUGUZI, WAKUNGA WAKUMBUSHWA JUU MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA.

    Akizungumza na TNMC Habari akiwa ofisini kwake jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma TNMC Bi.Happpy Massenga amesema Mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma ni mchanganyiko wa shughuli mbali mbali za mafunzo anayopata mtaaluma ili kujenga umahiri na kuimarisha uwezo wake wa kutoa huduma bora. Mafunzo haya yanajumuisha kujifunza kila siku mambo mbalimbali katika eneo la kazi kutokana na uhitaji, changamoto zilizopo au uwepo wa mambo mapya (updates) katika taaluma na huduma kwa ujumla.

    Mafunzo haya ni takwa la kisheria kwa wataalamu kufanya maendeleo endelevu ya umahiri wao wa kitaaluma kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010, Kanuni yake Kifungu cha 6 (28)(1) cha Kanuni ya mafunzo ya mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Training Regulations, 2010)

    Bi. Massenga amefafanua lengo la Mafunzo ya kujiendelni kitaaluma kwa wauguzi na wakunga yameandaliwa ili kuwawezesha kufanya maendeleo endelevu ya umahiri wao wa kitaaluma ikijumuisha;

    Kuboresha matokeo ya mgonjwa anayehudumiwa,Kurekebisha Makosa mengi yanayofanywa na wataaluma kwa sababu ya kukosa umahiri, ujuzi duni na mtazamo usiofaa dhidi ya taaluma na Makosa mengine yanatokana na uwepo wa teknolojia mpya katika huduma za Afya ambayo watendaji hawajaoneshwa au kujifunza.

    Kwa Upande wake msimamizi wa Mafunzo hayo Bi. Mwajuma Mutabazi amebainisha Umuhimu wa mafunzo ya kujiendeleza kuwa ni Kukidhi mapungufu yaliyobainishwa katika ujuzi na maarifa ya mtaaluma binafsi na Taasisi kwa ujumla, Kumwongezea Muuguzi/Mkunga maarifa,ujuzi pamoja na kumpa mtazamo mpya (Knowledge,Skills and Attitudes) katika utoaji wa huduma, Kumwezesha Mtaaluma kutoa huduma bora kwa wateja wake zinazoendana na wakati, Huwawezesha wataaluma kukabiliana na changamoto mbalimbali za kuibuka kwa magonjwa, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa haraka wa sayansi na teknolojia, Huinua kiwango cha kufiri na kufanya maamuzi ya kisayansi katika utoaji wa huduma, Humsaidia mtaaluma kukidhi takwa la Kisheria na kuweza kuhuisha leseni yake.

    Bi. Mwajuma amesema, Muda wa Mafunzo ya kujiendeleza yamegawanyika katika sehemu tatu ambapo alama 2- 40 zimetolewa moja, Mafunzo ya muda mfupi kuanzia saa moja mpaka mwezi
    Pili, Mafunzo ya muda wa kati kuanzia miezi 3 hadi 6
    Tatu ni  Mafunzo ya muda mrefu kuanzia mwaka mmoja na kuendelea.

    Hata hivyo, kutakuwa na Maboresho katika taratibu za mafunzo ( CPD logbook) ambapo, Kuanzia mwaka 2023 marejea ya mwongozo wa mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma yalifanyika ili kuendana na miongozo ya Wizara hivyo kupelekea kufanyika ambapo, Mtaaluma anatakiwa kupata alama 20 kila mwaka kutoka maeneo mbalimbali ya kujifunza katika mchanganuo ulioonyeshwa katika kitabu cha kuweka kumbukumbu (CPD Logbook) na Jumla ya alama za mafunzo anazotakiwa kupata mtaaluma ili kuhuisha Leseni yake ni 60 ndani ya miaka mitatu (2023 hadi 2025)

    Ikumbukwe kuwa, Mafunzo ya CPD yanapatikana kwa njia kadhaa yapo yale ambayo yanapatikana eneo la kazi ( non-accredited) ambayo mtaaluma anayapata kila siku eneo lake la kazi na yanapangwa na wataaluma wenyewe yakilenga kuboresha hali ya utoaji wa huduma na huduma kwa ujumla. Yanachukua asilimia 50 sawa na alama 30 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 10 kwa mwaka Pili, Mafunzo yaliyoratibwa na kupata itibathi ( Accredited CPD modules)  haya yameandaliwa na wadau mbalimbali kuanzia eneo la utoaji wa huduma na wanaosimamia miradi. Yanachukua asilimia 30 sawa na alama 18 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 6 kwa mwaka na Tatu, Mafunzo yanayopatikana kwa njia ya mtandao ( Online CPD) haya yanatolewa kupitia mtandao – mtaalamu anatakiwa kusoma maeneo yanayoongeza umahiri katika utoaji wa huduma. yanachukua asilimia 20 sawa na alama 12 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 4 kwa mwaka. Mtaaluma atasoma kupitia application ya WCEA (https://engagement.wcea.education/tnmc) na National e-leaning platform – ya Wizara ya Afya