Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limekutana na wadau kwa lengo la kutoa taarifa ya namna mtaala mpya ulivyoandaliwa na namna utakavyotumika. kikao hicho kimefanyika leo katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Saalam.
Mtaala uliokamilika tangu mwaka 2022 kwa uwezeshaji wa wadau wa maendeleo (UNFPA) ambaye ameonyesha umuhimu wa kuendelea kuboresha mafunzo ya taaluma ya Uuguzi na Ukunga nchini.
Mtaala ya Uuguzi na Ukunga umeandaliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyolinganishwa (Benchmarking) kupitia ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kutokana na hali ya utendaji unaotakiwa kwa wauguzi na wakunga.
Pia Mtaala umezingatia tafiti na maamuzi ya vikao mbalimbali vya kitaaluma, ambapo kwa sasa taaluma ya Uuguzi na Ukunga inakuwa kwa kasi na kufikia ngazi ya ubobevu (PhD) ambapo wanahitajika wataalamu wenye sifa zinazostahili na kuwezesha wataaluma kujiendeleza.
Hata hivyo, mtaala wa Uuguzi na Ukunga umeshapata idhini na Baraza la Uuguzi na Ukunga na kupewa idhibati na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi umechelewa kuanza kutumika kutokana na baadhi ya wadau kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya taratibu za uandaaji wa mitaala.
Watarajali zaidi ya 30 wamekutana Jijini Dodoma kwa lengo la kupata semina elekezi kabla ya kuanza mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za Afya hapa nchini.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Maadili, Usajili na leseni kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania imelenga kuwajengea uwezo wakutoa huduma kwa kuzingatia kanuni, Sheria na miongozo ya taaluma ya Uuguzi na Ukunga hapa nchini.
Akizungumza na watarajali Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga hapa Nchini Bi. Agnes Mtawa amewakumbusha watarajali hao kuzingatia taratibu za kiuuguzi na Ukunga sambamba na kuwataka kufanya tafiti katika kada hizo.
“Sasa mmeshatoka vyuoni mnakwenda kuhudumia jamii nendeni mkahudumie jamii huku mkufanya tafiti za kutosha katika kada ya Uuguzi na Ukunga hatutegemei ninyi kukaa nyuma nyuma mmeandaliwa, mmeiva sasa nendeni mkafanye kazi”- Bi. Mtawa.
Bi. Mtawa ameongeza kwa kuwataka watarajali kujitambua katika maeneo yao ya mafunzo huku akiwasisitiza kwenda kujifunza kwa vitendo.
Naye Mkurugenzi wa usajili, Leseni na Maadili TNMC Bi. Jane Mazigo amewasisitiza watarajali hao kuhakikisha wawapo katika maeneo ya kutolea huduma ni vyema kuzingatia miongozo ya sare, kanuni saba za maadili ya taaluma hiyo.
Aidha, Bi. Mazigo amewataka kuhudhuria siku zote zilizopangwa na Baraza bila ya kukosa ili kuhakikisha wanapata mafunzo mazuri ili kupata weledi wakutosha katika taaluma ya Uuguzi na Ukunga.
Wauguzi, Wakunga na Watoa huduma za Afya, wameagizwa kuendelea kubeba dhamana kubwa katika kuwapatia huduma bora Watanzania kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyowekeza katika sekta ya afya.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Festo Dugange wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wauguzi Viongozi Machi 26, 2025 Jijini Dodoma.
“Ninawaelekeza Wauguzi Viongozi wa ngazi zote kuimarisha usimamizi wa utoaji wa huduma bora ili wananchi wote wapate huduma bora na kwa Usawa, Tunatambua kuwa wauguzi wanafanya kazi nzuri sana japo kuna baadhi yenu wachache wanaharibu sifa nzuri ya wauguzi kwa kufanya makosa mbalimbali yanayoweza kuepukwa,” amesema Dkt. Dugange.
Ameongeza kuwa kuwa Serikali, imewekeza katika ngazi ya msingi pekee jumla ya Shilingi Trilioni 1.3 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake sambamba na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amepongeza ushiriki wa wauguzi katika mapambano ya magonjwa ya mlipuko hususani katika kuudhibiti ugonjwa wa Marburg nchini.
“Tunapozungumzia wauguzi na wakunga ni rasilimali watu ambayo inafikia asilimia 60 ya wataalam wote wa sekta ya afya na majukumu mnayofanya yanafikia asilimia 80. Huduma zote haziwezi kuboreka bila kuwa na rasilimali watu, inahitajika kuwa na watu wenye uwezo, weledi na ujuzi kama ninyi,” amesema Dkt. Magembe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mambo mbalimbali ya kada hizo kwani ilivyo sasa siyo sawa na miaka 10 iliyopita.
Hata hivyo,Msajili wa TNMC Bi.Agnes Mtawa akitoa salamu za shukrani kwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi. Amesema TNMC itajitahidi kupunguza malalamiko yote yanayohusu muuguzi na mkunga kwa kusimamia vyema taaluma hiyo hapa nchini.
“Ukizingatia uwekezaji wa Serikali katika upande wa Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa mazingira ya utoaji huduma sasa malalamiko madogo madogo juu ya wauguzi na wakunga yanakwenda kuisha kitakachobaki ni kupongezwa tu“ alisema Bi.Mtawa
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania leo 19 Machi 2025 limefanya maadhimisho ya miaka 72 Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1953.
Maadhimisho hayo ya kihistoria leo yamefanyika kwa kutembelea kituo cha watoto wenye ulemavu cha Mlali kilichopo wilayani Kongwa Dodoma.
Akizungumza katika hotuba yake kaimu Msajili TNMC Bi. Irene Chilewa amesema katika kipindi cha miaka 72 Baraza limepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi wauguzi na wakunga walisajiliwa ambapo na wenye madara mbalimbali ya elimu na hata nangazi ya Uzamivu PhD ambao jumla yao wamefikia taklibani 54,000, tofauti na miaka 72 iliyopita, kujenga mfumo wa TEHAMA, ujenzi wa ofisi za Baraza la Kibaha Mkoani Pwani na unaoendelea Jijini Dodoma.
“katika kuadhimisha siku ya Baraza tumekuwa tukitoa misaada na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii ambapo leo tumeleta mahitaji ya watoto yenye thamani ya Milioni Tano” amesema Bi. Irene
Naye Padri. Gaudence Aikaruwa, ambaye ni Mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na kutaja changamoto wanazokumbanazo katika malezi ya watoto hao ameshukuru Msaada huo ambao ni msaada mkubwa kwa sasa.
“Kituo kinawatoto zaidi ya 40 wanaolelewa mahali hapa, huu msaada utatusaidia sana Tunashukuru na Mungu awabariki” amesema Fr. Gaudence
Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.
Kila ifikapo tarehe 19 machi ya kila mwaka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Huadhimisha miaka siku ya kuanzishwa kwa taasisi hii.
Mwaka huu TNMC inatarajia kuadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake mnamo 19 machi 1953 kwa kutembelea na kutoa misaada ya kibinadamu katika kituo cha watoto walemavu cha Mlali kilichopo jijini Dodoma.
Lengo kubwa la kuadhimisha hivyo ni kurudisha shukrani kwa jamii kama Taasisi ilivyo na wajibu wa kutoa huduma bora kwa watanzania.
Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, anawataarifu wauguzi na wakunga wote waliopata sifa za kusajiliwa na Baraza baada ya kufaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 20.12.2024 kuwa, Mahafali ya 13 ya kutunuku Vyeti vya Usajili na Leseni yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 21.03.2025 kuanzia Saa 01:00 Asubuhi katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha UDOM (Chimwaga Hall) uliopo Jijini Dodoma. Aidha, kila mwanamahafali anatakiwa kuthibitisha ushiriki wake kwa kujisajili kupitia Tovuti ya Baraza www.tnmc.go.tz na kuhudhuria bila kukosa. Wanamahafali wote mnaelekezwa kuzingatia mambo yafuatayo; Kuvaa Sare ya Kitaaluma “Professional Uniform” iliyoidhinishwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga kama ifuatavyo: – • WANAWAKE- Gauni au Suruali na Blauzi rangi nyeupe ndefu. • WANAUME- Kaunda suti- Shati la rangi nyeupe na suruali rangi ya dark blue • VIATU- Vinavyofunika miguu na siyo vya wazi, viwe vya rangi nyeusi, nyeupe au brown. Kitambulisho cha Indexing, NIDA au Kitambulisho cha mpiga kura chenye picha ya mhusika/kinachomtambulisha. NB: Sandozi au Kandambili haviruhusiwi.
Kila ifikapo tarehe 19 machi ya kila mwaka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Huadhimisha miaka siku ya kuanzishwa kwa taasisi hii.
Mwaka huu TNMC inatarajia kuadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake mnamo 19 machi 1953 kwa kutembelea na kutoa misaada ya kibinadamu katika kituo cha watoto walemavu cha Mlali kilichopo jijini Dodoma.
Lengo kubwa la kuadhimisha hivyo ni kurudisha shukrani kwa jamii kama Taasisi ilivyo na wajibu wa kutoa huduma bora kwa watanzania.
Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania anawatangazia Watahiniwa wote wa kada za Uuguzi na Ukunga waliofanya Mtihani wa Usajili na Leseni tarehe 20.12.2024 na kufaulu kuwa, Mahafali ya 13 ya kutunuku Vyeti vya Usajili na Leseni yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 21.03.2025 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi katika Ukumbi utakaotangazwa hapo baadae. Hivyo, watahiniwa wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wa Mahafali ya 13 kwa kujisajili kupitia Tovuti ya Baraza www.tnmc.go.tz kuanzia leo tarehe 06.03.2025. Kwa ufafanuzi Zaidi wasiliana nasi kwa namba; 0736 006060.