ORODHA YA WATAHINIWA NA VITUO KWA MTIHANI WA VITENDO WATAALAMU WA DAWA YA USINGIZI NA GANZI (NURSE ANAESTHETIST)
GUSA LINK HAPA CHINI KWA KITUO CHA MLOGANZILA Orodha ya watahiniwa watakaofanya mtihani kituo cha MLOGANZILA GUSA LINK HAPA CHINI KWA KITUO CHA UPANGA Orodha ya watahiniwa watakaofanya mtihani kituo cha UPANGA
WATOA HUDUMA CHUMBA CHA UPASUAJI MTWARA-SZRH WANUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA TNMC.
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limetoa mafunzo elekezi kwa Madaktari, wauguzi,wakunga na wauguzi wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi wanaofanya kazi katika vyumba vya upasuaji pamoja na baadhi ya watumishi kutoka vitengo mbalimbali vya kutolea huduma wapatao 45 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, juu ya namna bora ya kutoa huduma […]
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA USAJILI NA LESENI ULIOFANYIKA TAREHE 23.08.2024
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa anawajulisha kuwa matokeo ya Mtihani wa usajili na leseni uliofanyika tarehe 23 Agosti, 2024 yametolewa tarehe 07 Novemba, 2024 baada ya kukamilisha mchakato wa taratibu za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga Tanzania ya mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act.2010). Taarifa […]
WATARAJALI WAPATA SEMINA ELEKEZI KABLA YA KUANZA MAFUNZO KWA VITENDO.
Watarajali zaidi ya 700 wamekutana katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Jijini Dodoma kwa lengo la kupata semina elekezi kabla ya kuanza mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za Afya hapa nchini. Semina hiyo iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Maadili, Usajili na leseni kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania imelenga kuwajengea uwezo wakutoa […]
TNMC YAZINDUA MFUMO WA MAWASILIANO KWA WATEJA
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) leo 11.10.2024 limezindua mfumo wa mawasiliano ya huduma kwa wateja utakao tumika kuwasiliana na umma hususani wadau wake wakuu ambao ni wauguzi na wakunga ndani na nje ya nchi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kilele cha wiki ya huduma kwa wateja. Wiki ya huduma kwa wateja ilianza tarehe […]
CHAMA CHA “WANAFIZIOTHERAPI” CHA ITEMBELEA OFISI YA MSAJILI TNMC.
Viongozi wa Chama cha “wanafiziotherapi” Tanzania (Association of Physiotherapists in Tanzania) leo oktoba 10,2024 wameitembelea ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Uunga Tanzania kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya utendaji kazi wa TNMC. Pamoja na mambo mengine mengi Viongozi hao ndg. Jerusalem Makotore(kulia) ambaye ni Mhazini na Dietrich Chussi(kushoto) ambaye ni katibu […]
‘Leseni Kwa Muuguzi, Mkunga ni Kibali Cha Utoaji Huduma- Bi.Jane Mazigo.
“Leseni ni utambulisho kwa muuguzi na mkunga kutoa huduma kwa jamii na ipo kwa mjibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 hivyo, ni vyema kwa Muuguzi na Mkunga kuwa na leseni iliyo hai muda wote wa kutoa huduma”. Hayo ameyasema Bi.Jane Mazigo, Mkurugenzi wa Maadili, Usajilina Leseni akizungumza na TNMC Habari mapema […]
TNMC Kuanzisha Kituo Cha Mawasiliano , Kuboresha Utoaji Huduma Kwa Mteja.
SASA KUTUMIA NAMBA MOJA YA MAWASILIANO. Katika kuboresha huduma kwa mteja, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TNMC linaendelea na mchakato wa kunzisha kituo cha mawasiliano na wadau wake hususani wauguzi na wakunga nchini na duniani kwa ujmla, machakato ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mapema mwezi huu Oktoba 2024. TNMC Inajenga mfumo huu wa […]
TNMC Yashiriki Mkutano wa ECSACON Lesotho
TNMC ikiwakilishwa na Msajili Bi. Agnes Mtawa, pamoja na maafisa waandamizi ambao ni Salome Kassanga na Irene Chilewa, imeshiriki Mkutano wa kimataifa wa kisayansi unaoratibiwa na jumuiya ya ECSACON nchini Lesotho kuanzia tarehe 11 hadi 13 Septemba 2024 kwa lengo la kubadilishana elimu, uzoefu na kuboresha utoaji huduma katika sekta ya Afya kwa nchi wanachama. […]
Msajili TNMC akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa TNMC mbele ya kamati ya Bunge.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchi Tanzania Bi. Agnes Mtawa akiwa na menejimenti yake, tarehe 06 Agosti 2024 aliwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Baraza mbele ya kamati ya Bunge inayosimamia sekta ya Afya na UKIMWI kupitia kikao kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge Bungeni Jijini Dodoma. Kamati hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti […]