Author: super-admin

  • Waziri Nape aipongeza TNMC kwa kudhamini Mkutano wa TBC.

    Waziri Nape aipongeza TNMC kwa kudhamini Mkutano wa TBC.

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ametoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi wa Mkutano. ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ukiwahusianisha watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ambao unafanyika Jijini Mwanza ambapo Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakiwa ni sehemu ya wadhamini wa mkutano huo.

    Mkutano huo uliobebwa na kauli mbiu ya “Vyombo vya Habari na Falsafa ya 4R” ikiwa na maana ya Mageuzi,maridhiano, ushahimilivu na kulijenga Taifa kwa kila Mtanzania kushiriki ili kulijenga Taifa letu.

    “Tumieni Mkutano huu kujifunza mambo muhimu kwa ajili ya kuhabarisha umma hasa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, ndio maana Serikali inaona kuna umuhimu wa kila idara ,Taasisi za Umma ziwe na Maafisa habari ili kuupa Umma taarifa hasa kujibu kero za wanajamii”-Waziri Nape.

    Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kimeshiriki Mkutano wa Mafunzo wa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia TBC ambapo Ezekiel M Nyalusi Afisa Uhusiano TNMC, amepokea Cheti cha pongezi ya udhamini wa mkutano huo kwa niaba ya Baraza.

    Mada mbalimbali zinazo husu utayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma zimetolewa katika mkutano ambao utatamatika tarehe 23 mwezi huu 2024.

    Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya 2010, na Kanuni zake kwa lengo la kuhakikisha huduma zitolewazo na wauguzi na wakunga zinaubora na salama kwa wateja.

  • Menejimenti ya TNMC imezuru eneo la Mradi wa Ujenzi.

    Menejimenti ya TNMC imezuru eneo la Mradi wa Ujenzi.

    Timu ya Uongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) inayoundwa na Msajili ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi, Wakurugenzi, Wakuu wa sehemu na Vitengo, mapema leo 21/02/2024, imezuru eneo ambalo unatekelezwa mradi wa ujenzi wa Ofisi za Baraza eneo la Medeli Jijini Dodoma.

    Ikumbukwe kuwa, mnamo tarehe 02/10/2023 Baraza lilitiliana Saini na kamapuni ya (SBS) kujenga Ofisi ya Baraza yenye hadhi ya ghorofa moja jengo ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka huu na kuanza kutumika, kisha badae Baraza litaendelea na ujenzi wa jengo kubwa la ghorofa nne.

    Imetolewa na; Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TNMC Dodoma

  • Wauguzi, wakunga wapata Mafunzo ya Sheria na Maadili-Geita

    Wauguzi, wakunga wapata Mafunzo ya Sheria na Maadili-Geita

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limeweka kambi ya siku sita mkoani Geita kwa lengo la utoaji Mafunzo ya Maadili na sheria ya Uuguzi na Ukunga kwa wauguzi na wakunga katika Halmashauri zote Mkoani humo.

    Ziara hiyo ya kawaida inalengo la kutoa elimu ya Maadili na Sheria kwa wauguzi na wakunga ili kuendelea kutoa Huduma kwa kuzingatia Maadili, Sheria, kanuni na taratibu ili jamii iweze kupata Huduma bora na Salama.

    Aidha, Akitoa mafunzo hayo katika halmasahauri ya Nyang’wale Mkoani Geita Msajili wa baraza hilo Bi.Agnes Mtawa amewapongeza wauguzi na wakunga Nchini kwa utoaji huduma bora kwa jamii, huku akibainisha kuwa takribani asilimia 60 hadi 80 ya watoa huduma za Afya Nchini, ni wauguzi na wakunga, hivyo ni vyema wakapata Mafunzo hayo ili kuendelea kuboresha zaidi Huduma za Afya Nchini.

    Kwa Upande wake Mwanasheria wa Baraza Bwana George Shilla, amewataka wauguzi na wakunga kujitokeza katika vituo vilivyopangwa kwaajili ya mafunzo hayo ili kuijua vyema Sheria hiyo ambayo inaiongoza Taaluma ya Uuguzi na Ukunga Nchini.

    Naye Bi. Mwajuma Mutabazi, ambaye ni muuguzi mbobezi kutoka Baraza amesema, ili kuwa muuguzi na mkunga mzuri ni vyema kuzingatia maadili ya taaluma hiyo huku ukitanguliza Utu katika utoaji Huduma.

    Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na Kanuni zake, kwa lengo la kusimamia wanataluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga, ili kuhakikisha jamii inapata Huduma za Afya zilizo bora na Salama.

  • TNMC Yatangaza Matokeo ya Usajili na Leseni

    TNMC Yatangaza Matokeo ya Usajili na Leseni

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika Tarehe 29.12.2024.

    Akitangaza Matokeo hayo katika Ofisi za Baraza Jijini Dodoma, Msajili wa Baraza Bi.Agnes Mtawa, amesema, Mtihani huo uliofanyika katika vituo nane (8) ambavyo ni Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Tandabui-Mwanza, Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi-Mbalizi, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu Stephano Moshi-Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St.John) – Dodoma, Chuo Kikuu cha Kampala-Dar es Salaam, Chuo cha Biashara -Dodoma (CBE) na Chuo cha Tabora Polytechnic.

    Jumla ya watahiniwa 2099 (50.7%) walifaulu mtihani huo kati yao watahiniwa 346 (72%) ni ngazi ya Shahada ya Uuguzi, 1737 (48%) ni Stashahada ya Uuguzi na Ukunga na watahiniwa 16 (30.8%) ni Astashahada ya Uuguzi na Ukunga.Watahiniwa 2043 (49.3%), walifeli mtihani huo, kati yao 136 (28%) ni ngazi ya Shahada (Digree) ya Uuguzi, 1871 (52%) ni Stashahada (Diploma) ya Uuguzi na Ukunga na 36 (69.2%) ni Astashahada( Cheti) ya Uuguzi na Ukunga.

    “Maswali ya mtihani huu yalichambuliwa kwa ngazi ya mafunzo ili kuona hali ya ufaulu wa watahiniwa katika maeneo ya umahiri uliopimwa kwa kuzingatia orodha ya vipimo vya umahiri na watahiniwa wengi walionekana kushindwa na kuwa nauelewa mdogo katika maeneo ya Misingi ya Uuguzi (Basic/ Fundamentals of nursing), tiba upasuaji na magonjwa ya dharura na mahututi (Medical Surgical Nursing and intensive care), Afya ya mama na mtoto (Midiwifery and Child Health), Afya ya Akili (Mental Health Nursing)” alitanabaisha Msajili huyo.

    Aidha, ameongeza kuwa, Katika Mtihani huu, hali ya Ufaulu inaonesha kunaongezeko la asilimia 4.7 ukilinganisha na mtihani uliofanyika mwezi Disemba, 2022 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 4.6. Ngazi ya Shahada ni 71%, Ngazi ya Stashahada ni 71% Ngazi ya Astashahada ni 56%
    Akihitimisha tarifa yake, Msajili Mtawa, amesema, Baraza litatoa mrejesho kwenye vyuo vya Uuguzi na Ukunga na vituo vya utarajali kuendelea kuongeza usimamizi wanafunzi ili kujifunza zaidi katika maeneo hayo.

    Baraza kwa kushirikiana na viongozi wa Uuguzi na Ukunga katika Mikoa na Wilaya (Supervisory Authority) kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa vyuo vya Uuguzi na Ukunga na usimamizi wa wanafunzi katika maeneo ya kujifunza kwa vitendo

    Baraza kufuatilia vyuo vya Uuguzi na Ukunga ili kubaini hali halisi ya uwepo wa mazingira ya ufundishaji katika hospitali na vyuo.
    Kufanya ufuatiliaji wa vituo vya mafunzo ya utarajali na vyuo ambavyo watahiniwa wameonyesha kupata ufaulu wa kiwango cha chini ili kubaini changamoto zinazowakabili.

    Wauguzi na wakunga hao wanatarajiwa kukabidhiwa chei cha usajili na leseni zao za kutambuliwa kwanye Mahafali maalum ya kitaaluma yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dodoma 23/02/2024

  • Kikao cha Baraza cha uendeshaji wa Mashitaka yanayowakabili wauguzi,wakunga chafanyika Jijini Dodoma.

    Kikao cha Baraza cha uendeshaji wa Mashitaka yanayowakabili wauguzi,wakunga chafanyika Jijini Dodoma.

    Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Prof.Lilian Mselle, ameongoza kikao cha Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kinachofanyika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

    Kikao hicho cha uendeshaji wa mashitaka huketi na kutolewa maamuzi kwa mujibu wa Sheria ya uuguzi na ukunga.

    Aidha, kwamujibu wa Sheria hiyo 31(1) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na uamuzi wa Baraza anaweza, ndani ya miezi mitatu toka tarehe ya kupata taarifa ya uamuzi, kukata rufaa kwa Waziri.

    (2) Waziri anaweza kutupilia mbali au kuruhusu rufaa yoyote au kubadili au kutofautiana na uamuzi wa Baraza au kutoa amri yoyote atakayoona inafaa.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya 2010, na Kanuni zake kwa lengo la kuhakikisha huduma zitolewazo na wauguzi na wakunga zinaubora na salama kwa wateja.

  • Baraza laendesha  Mafunzo ya Ushiriki utoaji Huduma katika Chumba cha Upasuaji kwa wauguzi na wakunga.

    Baraza laendesha Mafunzo ya Ushiriki utoaji Huduma katika Chumba cha Upasuaji kwa wauguzi na wakunga.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeendesha Mafunzo ya namna ya kushiriki utoaji huduma katika chumba cha upasuaji kwa wauguzi na wakunga katika Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma.

    Akitoa mafunzo hayo Afisa Muuguzi Mbobezi Kitengo Cha Upasuaji Bi. Salome Kassanga amewataka watumishi kuyazingatia yale waliyoyapata kutoka katika mafunzo hayo ili kuhakikisha jamii inapata huduma iliyo bora na salama.

    Kwa upande wake Muuguzi Kiongozi katika chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Mirembe Bi. Devotha Kimambo amelipongeza Baraza kwa Mafunzo hayo kuwa yatasaidia kuboresha mazingira ya vyumba vya upasuaji na kuwaongezea ujuzi watumishi hao

    Nao washiriki wa Mafunzo hao amemshukuru Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa kwa jitihada za utoaji wa mafunzo ya aina hiyo kwa watumishi waliopo kazini huku wakiiomba serikali irudishe mafunzo hayo yaliyositishwa ili kuboresha utoaji wa huduma ya aina hiyo kwa wateja mbalimbali.

    Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wauguzi na wakunga yanatarajiwa kuwa chachu ya utoaji wa huduma bora Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma.

  • WAUGUZI 81 WATUNUKIWA VYETI, LESENI ZA KITAALUMA LEO.

    WAUGUZI 81 WATUNUKIWA VYETI, LESENI ZA KITAALUMA LEO.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeandaa Mahafali kwa Wahitimu wa kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07.9.2023.

    Mahafali hayo ya tisa yamefanyika Jijini-Dodoma, ambapo wauguzi na wakunga wapatao 81 wametunukiwa vyeti pamoja na leseni za kutambuliwa rasmi kama wataalam wa kada hizo.

    Akizungumza wakati wa utoaji wa leseni za kitaaluma na Vyeti, Mgeni rasmi ambaye ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi na wakunga hao kwa hatua waliyoifikia ya kuaminiwa na Baraza na kuwataka kwenda kuhudumia jamii kwa kutanguliza Utu.

    “Tujikite katika kutoa Huduma bora kwa jamii, leo Baraza limeridhika na kiwango cha taaluma yako kwa kukupa leseni na cheti cha usajili wa Taaluma Mkaihudumie jamii kwa kufuata Sheria ya Uuguzi na Ukunga “-Bi.Agnes Mtawa

    Kwa Upande wake Mwanasheri wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Erasto Shilla, amewasihi wauguzi na wakunga kuzingatia Sheria ya Uuguzi na Ukunga wanapokuwa kazini ili kuepukana na adhabu ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria.

    Watahiniwa wa waliohitimu katika Mahafali hayo ya tisa ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni 81, ambapo ngazi ya Astashahada ni 32 na upande wa Shahada wakiwa ni 49.

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania chini ya Sheria ya Mwaka 2010 na kanuni zake (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa wateja.

  • MAHAFALI YA TISA YA TNMC WAUGUZI, WAKUNGA WATABASAMU

    MAHAFALI YA TISA YA TNMC WAUGUZI, WAKUNGA WATABASAMU

    Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeandaa Mahafali kwa Wahitimu wote wa Kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07/9/2023, Mahafali haya yaliyofanyika katika Ukumbi wa “CATHEDRAL SOCIAL HALL”Jijini-Dodoma
    yataambatana na utoaji wa Vyeti vya Usajili na Leseni.

  • TAARIFA YA MAHAFALI YA TISA YA KITAALUMA KWA WAUGUZI NA WAKUNGA.

    TAARIFA YA MAHAFALI YA TISA YA KITAALUMA KWA WAUGUZI NA WAKUNGA.

    Dodoma-Tanzania 09.01.2024.

    Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania anawaarifu Wahitimu wote wa Kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07/9/2023, Kuwa Mahafali ya kutoa Vyeti vya Usajili na Leseni yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 16/1/2024 kuanzia Saa1:00 Asubuhi katika Ukumbi wa “CATHEDRAL SOCIAL HALLJijini-Dodoma

    Maelekezo ya kufika Ukumbini,Ukumbi upo HAZINA, Mkabala na Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki-Dodoma, barabara inayotokea usawa wa geti la bima Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma kuelekea lango kuu la Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe.

    Washiriki wote mnatakiwa kuthibitisha Ushiriki wenu kwa kujaza fomu ya Mahafali kupitia Tovuti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga www.tnmc.go.tz.

    Hivyo, washiriki wote wa mahafali watatakiwa kuvaa Sare ya Kitaaluma “Professional Uniform iliyoidhinishwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga kama ifuatavyo: –

    1. WANAWAKE- Magauni au Suruali na Blauzi rangi nyeupe ndefu.
    2. WANAUME- Kaunda suti- Shati jeupe na Suruali dark blue
    3. VIATU– Vinavyofunika miguu na siyo vya wazi, viwe vya rangi nyeusi, nyeupe au brown.
    4. Kitambulisho chochote chenye picha ya mhusika  kinachomtambulisha

    Aidha, Katika Mahali haya Mada mbalimbali zitatolewa kisha Kiapo.

    NB: Sandozi au Kandambili haviruhusiwi. Kwa Mawasiliano zaidi piga namba 0655035078 na 0762003800

  • TNMC: Wauguzi, wakunga na watarajali 134 wamenufaika na Mafunzo ya Maadili DSM

    TNMC: Wauguzi, wakunga na watarajali 134 wamenufaika na Mafunzo ya Maadili DSM

    Jumla ya Wauguzi, wakunga na watarajali 134 wamenufaika na Mafunzo ya Maadili pamoja na uhamasishaji kuhusu Maadili katika Hospitali tatu ambazo ni Hosiptali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali tanzu ya Mloganzila na Hospitali ya Tumbi Kibaha Mkaoni Pwani.
    Mkurugenzi Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga kutoka Idara ya Usajili, Leseni na Maadili Bi. Jane Mazigo, ndiye aliyeiwakilisha Ofisi ya Msajili wa Baraza karatibu na kuendesha mafunzo hayo.
    Huu ni utaratibu wa kawaida wa (TNMC) katika kutekeleza majukumu yake ya kuzisimamia taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania.