
TNMC Kuanzisha Kituo Cha Mawasiliano , Kuboresha Utoaji Huduma Kwa Mteja.
SASA KUTUMIA NAMBA MOJA YA MAWASILIANO. Katika kuboresha huduma kwa mteja, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TNMC linaendelea na mchakato wa kunzisha kituo cha mawasiliano na wadau wake hususani wauguzi na wakunga nchini na duniani kwa ujmla, machakato ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mapema mwezi huu Oktoba 2024.